Serikali nchini Peru, imetangaza siku 30 za hali ya hatari nchi nzima, huku Waziri wa Ulinzi, Alberto Otarola akisema haki ya kukusanyika, kutoingiliwa majumbani na uhuru wa kutembea vimesitishwa.

Tangazo hili lililotolewa hapo jana Desemba 14, 2022 pia limeweka marufuku ya kutotoka nje usiku hatua ambayo inakuja wakati maandamano yakiendelea kwa siku kadhaa tangu kuondolewa madarakani kwa Rais Pedro Castillo na kutiwa nguvuni Desemba 7, 2022.

Wandamanaji wakikabiliana na Polisi nchini Peru ambapo Serikali imetangaza siku 30 za hatari. Picha ya MecroPress.

Hata hivyo, Castillo bado yuko jela kungojea mashitaka ya ufisadi na njama za uasi na aliyekuwa Makamu wake, Dina Boluarte, aliapishwa kuwa rais wa sita wa Peru baada ya Castillo kuwekwa kizuizini.

Boluarte amejaribu kuwashawishi waandamanaji kwa kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi, lakini hadi sasa hali haijatulia kutokana na Wafuasi wa Castillo na wapinzani wao kutaka uchaguzi wa haraka badala ya kumtambuwa Boluarte kama rais wao.

Kocha mpya Taifa Stars kutajwa mwaka 2023
Ten Hag aunga mkono Man Utd kupigwa bei