Tunaendelea na vikao ya maridhiano, vikao hivyo havizuii kujenga chama msiseme Mwenyekiti yupo kwenye maridhiano endeleeni na kazi za kujenga chama huku maridhiano yanaendelea.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na amendeleo (Chadema) Freeman Mbowe wakati akizungumza kwenye semina ya kuwajengea uwezo waliokuwa wagombea ubunge katika uchaguzi mkuu 2020 kupitia chama hicho.

”Nawashukuru viongozi wa chama ambao kwa njia moja ama nyingine mlishirikiana na viongozi hawa kuwezesha tukio hili kutokea siyo tukio la kawaida sana na katika historia yangu ya uongozi tulikuwa na utaratibu wa kukutana kama wabunge wa Chadema na kama siyo makandokando ya uchaguzi wa mwaka 2020”.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

“Lakini yalitokea yalitokea nisipoteze muda mrefu kuyazungumza hayo ila tuyachukue kama chachu kujiandaa na kututayarisha kutokupoteza muelekeo wa wapi chama chetu kinapaswa kwenda”. amesema Mbowe.

Nina hakika wengi wenu leo hii mngekuwa wabunge halali rasmi kabisa katika Bunge la Jamhuri na tungekuwa na kambi ya upinzani bungeni au pengine uchaguzi ungekuwa halali wote tungekuwa sehemu ya serikali wala siyo tu kambi ya upinzani bungeni.

Mtoto wa wiki mbili azikwa akiwa hai
TFF: Dirisha Dogo la usajili lipo wazi