Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kukamatwa kwa Oliva Meshack (19) mkazi wa Buseresere wilayani Chato mkoani Geita, kwa tuhuma za kumzika mwanae wa wiki mbili akiwa hai ili apate kwenda kujiuza.

Kamanda Safia Jongo, amesema kuwa anadaiwa kufanya kosa hilo kabla ya majirani kumtilia shaka na kuripoti kituo cha Polisi.

Aidha, amewaeleza waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 15, 2022 kwamba tukio hilo lilibainika baada ya majirani kutoa taarifa polisi.

”Jeshi la Polisi lilipata taarifa kutoka kwa wananchi, kwamba wanajua kunabint amejifungua mtoto lakini wanasiku zaidi ya tatu hawamuoni huyo binti hawamuoni huyo binti akiwa na mtoto wanatamaji wajue huyo binti amepeleka wapi huyo mtoto”

Baada ya kupata taarifa hiyo jeshi la polisi lilizungumza na huyo binti na kukiri nikweli alijifungua mtoto ambaye alikuwa na umri wa wiki mbili lakini kutokana na shughuli zake za kuuza baa na kujiuza mwili wake akaona huyo mtoto ni kero kwakwe na kuamua kuchimba shimo na kumzika akiwa hai”

Young Africans kuingia sokoni Dirisha Dogo
Mbowe: Tunaendelea na maridhiano