Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesema  Nchi za Afrika zimekua na kiwango kidogo cha biashara baina yake ukilinganisha na mabara mengine.

Takwimu zinaonesha Biashara baina ya nchi za Afrika ni 16.6% ya biashara zote za nje (exports) ukilinganisha na 68.1% baina ya nchi za ulaya, 59.4% baina ya nchi za Asia na 55.0% baina ya nchi za Amerika.

Ameyasema hayo wakati wa Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Kitaifa za Ubora kwa Washindi wa Msimu wa 2022/2023 ambapo  washindi wamekabidhiwa tuzo hizo na kuahidi kuendelea kuhamasisha uzalishaji na uuzaji wa bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora.

Kigae amesema serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iliona umuhimu wa kuanzisha Tuzo za ubora za Kitaifa na kutoa jukumu la kuziratibu kwa Shirika la Viwango Tanzania pamoja na TPSF kwa kushirikiana na Taasisi nyingine.

“Tuzo hizi ni sehemu ya mipango ya serikali katika kuboresha huduma na bidhaa zinazozalishwa nchini kupitia matumizi ya viwango na kanuni za ubora kwa taasisi za umma na sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa mifumo, bidhaa na huduma zinakidhi mahitaji ya kitaifa, kikanda na kimataifa na hivyo kufanya vizuri kwenye masoko ya ngazi zote hizo”. Amesema 

Aidha amesema washindi wa tuzo za ubora kitaifa mwaka wa 2021/2022 walishiriki katika mashindano ya kikanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Quality Awards) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Quality Awards).

“Matumizi ya Viwango, Udhibiti wa Ubora, ithibati pamoja na ugezi husaidia kulinda soko la bidhaa na huduma ndani ya nchi yetu na vilevile huboresha nafasi ya bidhaa na huduma zetu katika ushindani kwenye masoko ya kimataifa”. Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya amesema Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara imeendelea kujenga mazingira wezeshi kwa kamati inayoratibu tuzo za Kitaifa za Ubora ili kuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa na hivyo kupelekea ukuaji wa tuzo hizi ukilinganisha na misismu miwili iliyopita. 

Ameeleza kuwa wazalishaji na watoa huduma wanahitajika kujengewa au kujijengea utamaduni wa ubora na ushindani hapa nchini, ambapoa meeleza maandalizi ya tuzo hizo yalifanyika kwa ushirikiano wa karibu na taasisi mbalimbali ikiwemo, TPSF, CTI, SIDO, ZBS, TWCC, TCCIA, TANTRADE, SMIDA, TPSF pamoja na taasisi nyingine.

Serikali ya Uganda yaipiga JEKI The Cranes
Geita Gold yaichimba mkwara Simba SC