Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuenzi uhusiano wa kidini na kiutamaduni kati yake na Uganda.

Majaliwa amesema hayo alipomuwakilisha Rais Samia kati maadhimisho ya miaka 75 tangu ulipojengwa msikiti wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Makerere kilichopo Kampala nchini Uganda msiki huo ulifunguliwa na Mwanamfalme Abdullah wa Zanzibar mwaka 1948,

”Nyote mtakubaliana na nami kwamba uwepo wetu hapa ni ishara tosha ya kutambua umuhimu na mchango wa tukio hili la kihistoria katika kukuza mahusiano ya watu wetu hususa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki” amesema Majaliwa.

Msikiti wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda ulifunguliwa na Mwana wa Mfalme Abdullah wa Zanzibar 1948. 

Aidha Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Uganda na Chuo Kikuu cha Makerere katika kusimamia msikiti huo sambamba na kuruhusu waislam wa maeneo ya jirani kutumiakwaajili ya kuabudu.

Majaliwa ametoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kukemea mmomonyoko mkubwa wa maadili ambao umeshika hatamu.

”Katika hili naomba turejee manenoya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur’an tukufu sura ya 33 ayah 21 (Qur’an 33:21) kwamba ”Hakikia ninyi mnacho kiigizo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu”.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan   katika  maadhimisho ya  miaka 75 tangu ulipojengwa  msikiti wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Makerere Kampala, Uganda,

Ameongeza kuwa taasisi za elimu, jumuiya za dini, viongozi wa dini na viongozi wa umma wano wajibu wa kuilea jamii kwa kutoa elimu sahihiya mazingira sambamba na mafundisho sahihi na endelevu ya dini ili kuiwezesha kutambua na kufuata yote yaliyo mema kama tlivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na kuacha kabisa yote mabaya yanyomchukiza mwenyezi mungu.

”Nitumie fursa hii kuwaomba viongozi wa Jumuiya kuongeza juhudi katika kutoa mafunzo ya dini ili kujenga jamii yenye hofu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya maovu na hivyo, kupunguza au kuondoa kabisa mmompnyoko wa maadili tunaoshuhudia sasa”

Iringa yapaa Kimataifa uhifadhi wa Mazingira
Dkt. Mpango mgeni rasmi kongamano la uhifadhi wa mazingira