Mshambuliaji wa Klabu ya Brentford Ivan Toney amefunguliwa Mashataka mengine 30, akituhumiwa kujihusisha na Kamari kinyume na Kanuni za Soka nchini England.

Mshambuliaji huyo mwezi uliopita alifunguliwa Mashataka 232 ambayo anapaswa kuyajibu mbele ya Kamati ya Nidhamu ya Chama cha Soka nchini England ‘FA’, ili kujiondoa kwenye sakata la kujihusisha na Kamari kinyume na utaratibu.

Hadi sasa Toney mwenye umri wa Miaka 26, ameshaifungia Brentford mabao 10 katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ msimu huu 2022/23, lakini kwa mshangao mkubwa aliachwa kwenye kikosi kilichotajwa kushiriki Fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika nchini Qatar mwishoni mwa juma lililopita.

Kufuatia taarifa mpya ya mashtaka 30, Uongozi wa Klabu ya Brentford umethibitisha kukaa na Mshambuliaji huyo kwa ajili ya kujadili mambo kadhaa ambayo wanaamini yatweza kumuokoa na adhabu ya kufungiwa na Chama cha Soka nchini England ‘FA’.

“Klabu imechukua maamuzi ya kukaa chini na Ivan ili kuangalia namna gani ya kumsaidia kukwepa adhabu ambayo huenda ikamfanya akose sehemu ya Michezo ya Ligi Kuu msimu huu. Mzungumzo ya Pande hizo mbili yanaendelea.”

“Tutajitahidi kuufahamisha Umma wa Mashabiki wake na wa Klabu pia, ili kutuliza hali ya taharuki iliyojitokeza baada ya taarifa mpya ya Mashtka yanayomkabili Ivan.” imeeleza taarifa ya klabu ya Brentford

Toney amepewa muda hadi Jumatano (Januari 04-2023) kujibu tuhuma za mashataka mapya yaliyowasilishwa kwake kama anakubaliana nayo ama anayakataa, ili kupisha taratibu nyingine za kisheria kuchukua mkondo wake.

Mashtaka yaliyofunguliwa na FA dhidi ya Mshambuliaji huyo yamezingatia kifungu cha Kanuni E8, ambacho kinawabana Wachezaji wa Soka nchini England kujihusha na Mchezo wa Kamari kwa namna yoyote ile, ili kuepuka kashfa ya upangaji wa matokeo kutokea ndani ya Uwanja.

Endapo FA itamkuta na hatia Toney, huenda akakumbwa na adhabu ya kufungiwa kwa muda wa Majuma Kumi (10), kama ilivyowahi kutokea kwa Beki wa Kulia wa Newcastle United Kieran Trippier, Desemba 2020 baada ya kukutwa na hatia ya kutoa taarifa za uhamisho wake kutoka Tottenham kwenda Atletico Madrid ya Hispania.

BMTZ wakanusha kukwamisha pambano la Mwakinyo
Faru apewa jina la Waziri Mkuu