Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara, Abdurahman Kinana amesema Watanzania wanatarajia kuona mradi wa Bwawa la Nyerere utakapoanza usaidie kusambaza umeme kwa wingi na kwa gharama nafuu, huku akimpongeza rais Samia kwa kuhakikisha anaendeleza mradi huo.
Kinana ameyasema hayo hii leo Desemba 22, 2022 katika tukio la ujazaji maji katika Bwala la Mwl. Nyerere unaofanyika kwa kushuhudiwa na Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tnzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema, Utekelezaji huo wa mradi ambao ni moja kati ya ahadi zilizotolewa na CCM, pia utasaidia kutoa uhakika wa chakula kwa wananchi na kwarahisishia wakulima kufanya shughuli zao kwa uhakika na kuwasisitiza kutunza miundombinu inayowazunguka na kufanya kilimo cha umwagiliaji chenye tija.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Jmhuri ya Muungahno wa Tanzania Dkt. Tulia Akson amesema Bunge litajitahidi kutoa ushirikiano katika ufanikishaji wa mambo yote ya msingi ambayo yatasaidia kuinua pato la Mtanzania na Taifa kiujumla.