Jumla ya Wafungwa 12, wamefariki dunia katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu, ndani ya gereza kuu la mji wenye madini mengi wa Kamituga uliopo Mkoa wa Kivu Kusini.

Mbali na tukio hilo la vifo, pia Hospitali ya Kamituga imewapokea wafungwa wengine 31 walioambukizwa ugonjwa huo kwa ajili ya kupatiwa matibabu, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakisema mbali na ugonjwa pia wafungwa wanakosa chakula na afya zao kudhohofika.

Polisi na Askari Magereza wakiangalia dirisha ambalo wafungwa walitumia kutoroka. Picha ya Daily Sabah.

Waziri wa Afya wa jimbo la Kivu Kusini, Masine Kinenwa amesema kwasasa juhudi zinafanyika ili kudhibiti kipindupindu kwenye eneo hilo na kwamba juhudi za watoa huduma zinaendelea ili kuwanusuru watu wengine wasio na maambukizi na kutangaza tahadhari ya masuala ya afya katika eneo hilo.

Aidha, Kinenwa amesema kuna ujumbe wa madaktari toka idara ya afya umeelekea Kamituga ukiambatana na madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, maafisa wa Shirika la Afya Duniani, WHO, pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto, UNICEF, wakikabiliana na hatua za kuudhibiti ugonjwa huo.

Bwawa la Nyerere: Rais Samia amtaja Magufuli, shangwe laibuka
Bodi ya Wakurugenzi TAWA yafanya ziara ya kikazi Pori la akiba Kirejeshi