Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto, UNICEF iliyotolewa Alhamisi (Desemba 22, 2022), imesema zaidi ya watoto milioni 20, wapo katika hatari ya njaa, kiu na magonjwa katika nchi za Ethiopia, Kenya na Somalia kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi, migogoro, mfumuko wa bei na uhaba wa nafaka ulioathiri pakubwa eneo la Pembe ya Afrika.

Ripoti hiyo inasema, Watoto hao walikuwa milioni kumi mwezi Julai, 2022 na sasa wamefikia milioni 20.2 ikiwa ni zaidi ya mara mbili, licha ya juhudi za mashirika ya kibinadamu kupunguza baadhi ya athari mbaya zaidi za kile kilichohofiwa kama alivyobaini Naibu Mkurugenzi wa UNICEF katika Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Lieke van de Wiel.

Watoto wakisukuma madumu ya maji ukanda wa Pembe ya Afrika. picha ya Prensa Latina.

Aidha, iema takriban watoto milioni mbili nchini Ethiopia, Kenya na Somalia wanahitaji matibabu ya haraka kutokana na utapiamlo uliokithiri, na kwa kuzingatia uhaba wa maji, familia zinakabiliwa na hali mbaya hali inayoongeza shinikizo kwa watoto, pamoja na unyanyasaji, kazi ya kulazimishwa, ndoa, ukeketaji, unyanyasaji wa kijinsia na usio wa kijinsia hasa wasichana wadogo.

Kutokana na hali hiyo, UNICEF ​​​​imetoa wito wa michango kiasi cha dola Milioni 759 ili kukidhi mahitaji katika mwaka ujao wa 2023 na inakadiriwa kuwa zinahitajika Dola milioni 690 za ziada zinaweza kuwezesha watoto na familia zao, ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.

"Wasanii mkikopa lazima mrudishe"- Mjata
Prof. Mbarawa ataja maelekezo ya Rais Samia