Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema uhuru wa Habari uliopo nchini, unapaswa kulindwa kisheria, ili wanahabari waendelee kufanya kazi bila wasiwasi.
Balile, ameyasema hayo katika Kongamano la Kwanza la Maendeleo ya Sekta ya Habari lililofanyika Jijini Dar es es Salaam, na kubainisha kuwa mabadiliko ya vipengele vya sheria ya habari yatafikishwa Bungeni Januari 2023.
Amesema, “Wadau wa habari nchini wanafurahia uhuru wa habari uliopo nchini, tunaamini serikali italinda uhuru huu kisheria katika Mabadiliko ya Sheria ya Habari yajayo.”
Aidha, amefafanua kuwa “Nimezungumza na Waziri Nape (Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) kuhusu mjadala wa Sheria ya Huduma za Habari, amesema Januari (2022) mapendekezo yatafikishwa bungeni.”