Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ kupitia Kamati ya Sheria, na Hadhi za Wachezaji, limemwita Kiungo Mshambuliaji kutoka Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kwa ajili ya mazungumzo ya kusaka suluhu kati yake na Uongozi wa Young Africans.

Pande hizo mbili zimeingia katika Sintofahamu, kufuatia Kiungo huyo kudaiwa kuvunja mkataba kwa kulipa gharama ya sehemu ya mkataba wake ambao ulitarajiwa kufikia tamati mwaka 2024.

TFF imethibitisha kumwandikia Barua ya wito ‘Fei Toto’ ambaye imethibitika yupo Falme za Kiarabu kwa mapumziko na kufanya mazoezi Binafsi kwa ajili ua kujiweka Fit katika kipindi hiki ambacho yupo nje ya kambi ya Young Africans.

Barua hiyo imemtaka Feisal kufika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kesho Jumatano (Januari 04) saa nne asubuhi katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’.

Wakati huo huo Feisal Salum ‘Fei Toto’ anaendelea na mazoezi binafsi humo Falme za Kiarabu wakati huu ambao hayupo na kikosi cha Young Africans.

Fei Toto akiwa huko Uarabuni amekuwa chini ya Mwalimu (Trainer) ambaye huwa anawanoa mastaaa wengi kutoka Ulaya akiwemo mshindi wa Ballon D’Or Karim Benzema, Antonio Rüdiger, Benjamin Mendy na wengine wengi.

Kipindupindu: Watu 10 walazwa Hospitali
Vifo 32 matukio ya uokoaji, Zimamoto wataja sababu