Saa chache baada ya kukamilisha taratibu za kusani mkataba mpya wa miaka miwili, Mlinda Lango chaguo la Kwanza katika kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young
Africans Djigui Diara ametoa kauli ya kibabe.

Mlinda Lango huo kutoka nchini Mali alisaini mkataba mpya Young Africans usiku wa kuamkia leo Jumanne (Januari 03) jijini Dar es salaam na baadae kuelekea nchini kwao kwa mapumziko wa majuma mawili.

Diara amesema kitendo cha kukubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Young Africans ni kutaka kupambana zaidi ya ilivyokuwa katika miaka miwili ya awali.

Amesema anaamini alipo ni mahala salama na ni sehemu ya ndoto za Wachezaji wengi wa ndani na nje ya Tanzania kuitumikia Young Africans ambayo amesisitiza ni Klabu Bora Barani Afrika kwa sasa.

“Young Africans ni klabu kubwa Afrika na bila shaka ni ndoto ya wachezaji wengi kucheza hapa. Niwaahidi mashabiki wa Young Africans kuwa nitaendelea kujituma na kuhakikisha timu yetu inafanya vyema kwenye michuano ya ndani na Kimataifa,” amesema Diara

Mlinda Lango huyo mwenye umri wa miaka 27, alisajiliwa Young Africans mwanzoni mwa msimu uliopita 2021/22 akitokea nchini kwao Mali alikokuwa anakipiga na Klabu ya Stade Malien.

Mudathir Yahya amfuata Sure Boy Young Africans
Roberto Oliveira Bosi mpya Simba SC