Aliyekuwa Kiungo wa Azam FC Mudathir Yahya Abbas ametambulishwa rasmi kuwa Mchezaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans.

Kiungo huyo aliyeamua kuachana na soka la ushindani baada ya kuachwa na Azam FC mwishoni mwa msimu uliopita, ametangazwa kuwa MWANANCHI leo Jumanne (Januari 03) majira ya saa kumi jioni.

Mudathir anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kutambulishwa na Young Aficans katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, akisaini mkataba wa miaka miwili kwa mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi.

Mudathir anaungana na mastaa wenzake wa Azam winga Farid Mussa na kiungo Salum Aboubakar ‘Sure boy.

Usajili huo unaifanya Young Africans kuwa na viungo wanne wa ukabaji wakiwemo Zawadi Mauya, Khalid Aucho, Gael Bigirimana na kiraka Yannick Bangala.

Young Africans imeipiga bao Simba SC katika usajili huo ambao nao waliwahi kutamani huduma ya kiungo huyo Mzanzibar.

Huyo anakuwa mchezaji wa kwanza mpya kwa Yanga kumsajili katika dirisha dogo huku wengine wawili watatu wakifuatia ingawa uongozi wa klabu hiyo unafanya siri.

Dkt. Samia: Ruksa mikutano ya hadhara
Djigui Diara atamba kibabe Young Africans