Chama cha United Democratic Party (UDP) kimesema wakati wowote watakapokuwa tayari wataanza mikutano ya hadhara mara baada ya Rais Samia kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa baada ya kuzuiwa kwa muda wa miaka 6 na kwamba Wananchi wataamua nini wanataka.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho, John Cheyo wakati akizungumza na dar24 Media na kubainisha kuwa, anakubaliana na maoni ambayo yametolewa na wengi na kwamba jambo hilo linaanzisha ukurasa mpya hivyo watu wote walipokee na wampongeze Rais kwa uamuzi huo.

Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (UDP), John Momose Cheyo.

Aidha, Cheyo alipoulizwa ni lini Chama chake kinataraji kuanza mikutano hiyo, akajibu kuwa, ”Wewe umeambiwa jana ruksa mikutano ya hadhara, utaanza kusema nitaanza kesho, tutakapo kuwa tayari tutaanza mikutano ya hadhara, kuna wengine ambao wataanza na kuna wengine ambao watachelewa ni fursa na unatumiaje hiyo fursa ya mikutano ya hadhara.”

Kuhusu vyama vya siasa kuwa na ukata wa kifedha na hivyo kuwa na hofu ya kuweza kumudu hekaheka za mikutano ya hadhara, Cheyo amesema, ”Wananchi wanauamuzi kama mikutano ya hadhara tunafanya maonyesho ndiyo itahitaji fedha lakini kama wanataka kusikia mawazo ambayo yanatokana na vyanzo mbali mbali kama vile tulivyoanza mwanzoni basi hii fursa ya wao kusikiliza.”

Matusi kwenye Mitihani tatizo ni mazingira: Mwanasaikolojia
Rais Biden awashangaa Wabunge, asema ni aibu