Kufuatia Baraza la mitihani nchini NECTA, kufuta matokeo ya wanafunzi 14 ambao waliandika matusi katika mtihani wa upimaji wa kitaifa kidato cha pili mwaka 2022, Mtaalamu wa Saikolojia, Justus August ameelezea sababu zilizopelekea kuandika vitu visivyofaa, kwenye mtihani ikiwemo matusi.

Akizungumza na Dar24 Media, August amesema kuwa matusi ni miongoni mwa tabia ambazo zinamuendelezo kutokana na mazingira mtu aliyokulia na namna mtu alivyojifunza kwenye kukabiliana na nyakati.

Amesema, “Ukiona mtu anaandika matusi au anabisha kwa kutoa lugha ambazo haziendani na maadili au utamaduni wa eneo fulani ujue anasumbuliwa na mazingira aliyokulia na kwa mwanafunzi aliyeingia kwenye mtihani akakutana na maswali magumu au walimu walikuwa wakimtishia sana anaona yupo sehemu ya kutoa yake ya moyoni.”

August anasema ukiona mtu anaandika matusi au anabisha kwa kutoa lugha ambazo haziendani na maadili au utamaduni wa eneo fulani ujue anasumbuliwa na mazingira aliyokulia. Picha ya Denilson Odhiambo / Alliance.

Ameongeza kuwa, “Hili ni tatizo la kitabia kwasababu saikolojia ina husiana na tabia hili linaweza likawa ‘delt’ au tukalishughulikia kupitia smafunzo ya saikolojia kwa namna ya kumufanya ajue naman ya kuishi na watu lakini namna ya kuzimudu hisia kwa nyakati zile ambazo anakuwa anapitia.’’

“Hawa wanaokosea ni wachache ambao tunaweza kuwaona lakini huko mtaani wapo wengi, kuna baba anamtukana mama, mama anamtukana mwanae lakini kuna watu wazima wanasema wanataniana lakini wanaongea kwa kutukanana matusi kwa hiyo mfumo unatakiwa kugusa pakubwa usiishie tu kwa hawa waliofanya mtihani na kuwalalamikia wao hawa ni zao la wengi waliopo huko katika mazingira ambayo wamekuliwa.’’ amebainisha August.

Hata hivyo amebainisha kuwa, “Tukiwatafuta hawa inaweza ikawa ni sahihi lakini tunawatafuta kuokoa nini kwanini tusiende kwenye chanzo watu waandaliwe kutokea kwenye familia lakini waliopo kwenye familia waandaliwe kwaajili ya kulea familia.”

Majaliwa akubali maboresho ujenzi Hospitali Namtumbo
Mikutano ya hadhara: Wananchi wataamua