Kikosi cha Simba SC kilichoweka Kambi mjini Dubai-Falme za Kirabu kitacheza Michezo miwili ya Kirafiki kabla ya kurejea nchini Tanzania kuendelea na Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba SC imeweka kambi mjini humo tangu Jumapili(Januari 08), chini ya Benchi lake la Ufundi linaloongozwa na Kocha kutoka nchini Brazil Robert Oliviera ‘Robertinho’.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyochapishwa kupitia SimbaAPP, Kikosi cha Klabu hiyo kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi Klabu ya Al Dhafra FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kirabu ‘UAE Pro League’.
Mchezo huo utachezwa January 13, 2023 saa 11:00 jioni.
Mchezo wa Pili wa Kirafiki utakuwa dhidi ya dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi, utakaochezwa January 15, 2023.
CSKA Moscow wamewahi Kuwa Mabingwa wa UEFA Europa League Msimu wa 2004-05, wakiifunga Sporting Lisbon ya Ureno.
Mchezo wa pili Simba SC itakucheza dhidi ya Klabu ya Al Dhafra FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kirabu ‘UAE Pro League’.
Kambi ya Simba mjini Dubai-Falme za Kiarabu imelenga kujiandaa na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi itakayoanza rasmi mwezi Februari.
Simba SC imepangwa Kundi C sambamba na Mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers SC, Horoya AC (Guinea) na Raja Casablanca (Morocco).
Hata hivyo baada ya kurejea jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma hili, Simba SC itaendelea na Mshike Mshike wa Ligi Kuu, kwa kucheza mchezo wa Mzunguuko wa 20 dhidi ya Mbeya City, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumanne (Januari 17).