Rais wa Heshima na Mwekezaji Mwenza wa Klabu ya Simba SC Mohamed Dewji Mo, ni kama ameibua shangwe kwa Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo, baada ya kugusia kwa uchache usajili wa Dirisha Dogo.
Mo Dewji ambaye kwa sasa yupo Dubai, jana Jumanne (Januari 11) alitembelea Kambi ya kikosi cha Simba SC na kuzungumza na Wachezaji na Benchi la Ufundi linaloongozwa na Kocha kutoka nchini Brazil Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’.
Tajiri huyo ametumia ukurasa wake wa Mtandao wa Twiter kuandika ujumbe unaothibisha kufanyika kwa usajili wa Wachezaji wanaowaniwa Simba SC katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo.
Mo ameandika: Habari za asubuhi Mashabiki wa @SimbaSCTanzania. Usajili umefika pazuri #NguvuMoja
Hadi sasa Simba SC imemsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza akitokea Geita Gold FC, na tayari ameshacheza mchezo mmoja wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons.
Kwenye mchezo huo uliopigwa Desemba 30-2022 Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, John Bocco na Saido walifunga mabao matatu ‘Hat Trick’ kila mmoja , huku Shomari Kapombe akifunga bao moja.