Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ na Kampuni ya kutengeneza vifaa vya Michezo ya Umbro wamezindua Mpira rasmi wa michuano ya Fainali za Mataifa Bingwa Barani humo ‘CHAN’ 2023.
Fainali hizo ambazo hushirikisha wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (Mataifa yao) zimepangwa kuanza kuunguruma kesho Ijumaa (Januari 13) nchini Algeria.
Mpira huo Maalum umepewa jina la ‘Marhaba’ ikiwa na maana ya ‘Karibu’.
Mwenyeji wa Fainali za ‘CHAN’ Algeria anatarajiwa kucheza mchezo wa ufunguz i dhidi ya Libya kesho Ijumaa, majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Timu hizo zipo Kundi A lenye timu nyingine kama Ethiopia na Msumbiji.
Kundi B: DR Congo, Ivory Coast, Uganda na Senegal
Kundi C: Ghana, Madagascar, Sudan na Morocco
Kundi D: Angola, Mali na Mauritania
Kundi E: Cameroon, Congo Brazzaville na Niger
Fainali hizo zinatarajiwa kufikia tamati kwa mchezo wa Fainali utakaopigwa Februari 4, 2023.