Klabu ya Young Africans inatajwa kukaribia kukamilisha dili la kumnasa beki wa Kimataifa kutoka nchini Mali na Mabingwa wa Ligi Kuu Nchini humo Stade de Malien, Mamadou Doumbia.

Young Africans imedhamiria kumalizana na beki huyo mwenye umri wa miaka 27 kabla Dirisha la Usajili halijafungwa Jumatatu ya juma lijalo.

Beki huyo huenda akatangazwa rasmi kwa Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo Kongwe nchini Tanzania sambamba na Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Kennedy Musonda ambaye Usajili wake umeshakamilika.

Doumbia kwa sasa yupo kwenye Kikosi Cha Mali kinachoshiriki Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ zitakazoanza rasmi baadae leo Ijumaa (Januari 13) nchini Algeria.

Beki huyo amewahi kucheza na Mlinda Lango Djigui Diarra wakiwa kwenye Kikosi Cha timu ya Taifa ya Mali na Klabu ya Stade de Malien.

Ismael Sawadogo anukia Simba SC
TPLB yasogeza mbele mchezo namba 157