Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando amefika katika eneo liloathiriwa na mafuriko leo Ijumaa Januari 13, 2023  eneo la Kihonda mahali ambako wananchi wameathirika zaidi huku akisaidia kuokoa watu na mali zao.

Hata hivyo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wapo kwenye maeneo mbalimbali Manispaa ya Morogoro wakiendelea kuokoa watu na mali zao.

Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro kuanzia saa 9 alfajiri, zimesababisha madhara mbalimbali kwa wakazi wa mkoa huo ikiwa ni pamoja na mafuriko na foleni ya magari Barabara kuu ya Morogoro kwenda Dodoma.

Hata hivyo, mvua imeendelea kunyesha na uokoaji unafanyika.

TPLB yasogeza mbele mchezo namba 157
Migogoro ndani ya ndoa yapata tiba kamilifu