Uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 5 kwa mwaka 2023 ikilinganisha na mwaka 2022, ambapo ulikua kwa asilimia 4.7 na mwaka 2021 kwa asilimia 4.3 ulipopungua kwa nukta 4.
Hayo, yamebainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.
Amesema ni matarajio yake kuwa uchumi utazidi kukua kutokana na usimamizi mzuri wa uchumi ambapo Tanzania imetajwa na Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Afrika.
Rais Samia ameongeza kuwa, usimamizi huo unatokana na mabadiliko mbalimbali yaliyolenga kubadilisha mazingira ya kibiashara yaliyohamasisha sekta binafsi kurejesha masoko hivyo kupelekea kuongezeka kwa uwekezaji wa moja kwa moja nchini.Â