Baada ya December 14, 2022 kupitishwa sheria na Baraza la Wawakilishi na kusainiwa na Rais wa Zanzibar kisha mchakato kuanza wa kuibadilisha Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), hatimaye jambo hilo limekamilika na sasa inaitwa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).

Mkuu wa ZRA, Yussuph Juma Mwenda amesema mamlaka hiyo itashirikiana na walipa kodi ili kuhakikisha kila Mfanyabiashara analipa kodi inayotakiwa na kwamba mamlaka hiyo haipo kwa ajili ya kumkandamiza yeyote.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Saada Mkuya (kushoto) akiwa na Kamishna wa ZRA, Yussuf Juma Mwenda wakati  akitangaza mabadiliko ya ZRB kuwa ZRA.

Aidha, amemuhakikishia Rais Mwinyi kuwa ZRA  na Watendaji wake watahakikisha wanatimiza matarajio husika na kwamba wote wenye stahili ya ulipaji kodi watashiriki zoezi hilo na kwamba kwa kipindi cha miezi sita, wanajipanga kukusanya Shilingi 300 bilioni kutoka Shilingi 293 bilioni za awali sawa na wastani wa ukusanyaji wa Shilingi 500 milioni kwa mwezi.

Januari 13, 2023, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dkt. Saada Mkuya akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisi za mamlaka hiyo Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi alisema mabadiliko hayo ya ZRB kuwa ZRA yanatarajia kuongeza weledi wa watumishi.

Madereva waungana kupinga ukatili wa Kijinsia
Mwanaharakati na Spika wa Bunge la kwanza afariki Dunia