Serikali ya nchi ya Chad, imeondoa marufuku na kuruhusu vyama vya siasa vya upinzani kuendelea na shughuli zake, ikiwemo mikutano ya kisiasa.
Marufuku hiyo, iliwekwa baada ya kutokea kwa maandamano ya wapinzaji jijini Ndjamena na miji mingine dhidi ya serikali mwaka uliopita (2022).
Katika maandamano hayo, Polisi walitumia nguvu kupambana na waandamanaji na kuwakamata baadhi ya wanasiasa wa upinzani huku wengine wakitoroka, kitendo ambacho kililaaniwa na jumuiya ya Kimataifa.
Mamia ya watu walipoteza maisha katika maandamano hayo, na Waziri wa Mambo ya ndani, Limane Mahamat, amesema wanasiasa wa upinzani sasa wanaweza kuendelea na shughuli zao ili mradi wafuate sheria za nchi.