Mbunge wa viti maalum CCM, Khadija Shaaban, amesema hali ya watoto wenye ulemavu nchini ni mbaya kuliko inavyodhaniwa, na kwamba juhudi za dhati zinahitajika katika kuliangalia suala hilo ili kuwaokoa na magumu wanayopitia.
Keisha ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa wazazi wanaojifungua watoto wenye ulemavu wanapata shida na wana hali ngumu kutokana na baadhi ya wanafamilia na wazazi wenza kuwatenga aina ya watoto hao.
Amesema, akina mama wengi wamekuwa wakitelekezwa na wenza wao kutokana na kupata watoto wenye ulemavu, kitu ambacho huwafanya wawe wakiwa, na kuiomba Serikali kumfikiria mzazi ambaye hana uwezo wa kufanya kazi yoyote kutokana na kumlea mtoto mwenye ulemavu.
Aidha, amesema Serikali pia iangalie namna ambayo inaweza kumsadia kiuchumi mlezi wa aina hiyo ili awqeze kumudu gharama za maisha ya kumhudumia mtoto mwenye ulemavu iliwemo kutoa kipaumbele katika baadhi ya mambo ikiwemo matibabu.