Kocha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara na Washiriki wa Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika Young Africans Nasreddine Nabi, amefunguka ubora wa kikosi cha US Monastir.

Young Africans itakua mgeni wa US Monastir Jumapili (Februari 12), katika Uwanja wa Hammadi Agrebi, mjini Tunis, majira ya saa moja usiku kwa saa za Tanzania.

Kocha Nabi amefunguka ubora wa wapinzani hao, baada ya kufuatilia michezo yao miwili ya Ligi Kuu ya Tunisia dhidi ya EO Sidi Bouzid na kisha Rejiche, akiwa sehemu ya watazamani.

Kocha huyo aliyetangulia nchini Tunisia kabla ya safari ya kikosi chake ambacho tayari kimeshawasili mjini Tunis, amesema wana kazi ya kuwachunga mastaa wanne wa timu hiyo watakaovaana nao, mwishoni mwa juma hili.

Amefichua kuwa wapishi wa US Monastir ni Mabeki wao wawili wa pembeni, akiwataja wengine kuwa ni Kiungo wa Kati na Nahodha wao huku pia wakiwa na Mshambuliaji anayejua kufunga kwa vichwa katika safu ya ushambuliaji.

“Tunatakiwa kuwa makini na hao wachezaji wanne, timu yao inategemea ubora wao katika kutengeneza mashambulizi lakini mtu wa kumalizia ni huyo mshambuliaji wao, tutatafuta akili ya jinsi ya kuwadhibiti.” amesema Kocha Nabi

Kikosi cha Young Africans kinatarajia kuanza mazoezi nchini Tunisia leo Alhamis (Februari 09), chini ya Kocha Nabi, huku wakiamini muda wa kufanya hivyo utatosha kabla ya kuingia dimbani Jumapili kuikabili US Monastir.

Mwamnyeto: Ni ngumu kupata ushindi ugenini
Simba SC yatajwa kila kona Conakry