Nchini Msumbiji mamlaka bado inashughulikia athari za mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika jimbo la Maputo wiki hii.

Vyanzo vya ndani viliripoti kwamba takribani familia 2,400 zimeathiriwa, mafuriko hayo yaliathiri kitongoji cha Matola na wilaya ya Boane karibu na mji mkuu, wa Maputo.

“Nyumba zetu zimejaa maji, hatuna pa kulala, ghala yetu ilienda na mvua, hatuna chakula, watu wanaburuzwa na maji, nyumba ziko nyingi Caful, zote ziko chini. majini, hakuna mashua inayoweza kuwaokoa watu hao, tunaomba msaada wa helikopta au boti”, Lurdes Simão Dove, mwathirika wa mafuriko aliyeokolewa kutoka wilaya ya Boane.

Baadhi ya wathirika wa mafuriko waliokolewa

Katibu wa Kwanza kutoka wilayani Boane Adolfo Mate, alisema kuwa “Kuanzia jana hadi leo tumeokoa zaidi ya watu mia moja na leo tunatarajia kuokoa zaidi ya watu 300”.

Hata hivyo mafuriko zaidi yanatarajiwa katika Mkoa wa Maputo huku maji kutoka mito iliyofurika nchini Afrika Kusini na Eswatini yakielekea chini.

Mafuriko hayo yaliathiri kitongoji cha Matola na wilaya ya Boane

LIVE: Meli ya MV Mwanza ''Hapa Kazi Tu'' yashushwa majini
Rais Samia aongeza 'boom' kwa wanachuo