Wanahabari nchini El Salvador, wamelalamikia kitendo cha Rais wa nchi yao, Nayib Bukele kutowajali na kutoheshimu uhuru wa vyombo vya Habari.

Bukele anadaiwa kufanya mikutano na wanahabari kwa nadra na mara nyingi hupendelea kutumia mtandao wa Twitter kutoa taarifa zake.

Rais wa El Salvador, Nayib Bukele. Picha ya CNN.

Inadaiwa kuwa, licha ya kutojali kuulizwa maswali kuhusu sera zake, wachambuzi wanasema Rais Bukele pia huwa haiti vyombo vya habari ambavyo humkosoa yeye na serekali yake.

Hata hivyo, vyombo vingi vya Habari nchini humo vimejikita katika kuripoti masuala ya rushwa, ikiwa ni pamoja na inayolenga shutuma za kujihusisha kuanzia utakatishaji fedha mpaka utoaji wa ripoti za uongo.

Serikali yahimiza ushirikiano utendaji kazi
Majaliwa awataka wakuu wa idara kusimamia miradi