Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Nabi amesema, unyumbulifu wa kikosi chake katika Michezo ya Kimataifa na Ligi Kuu, unampa jeuri ya kuamini wana uwezo wa kufanya vizuri kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Real Bamako.

Young Africans itacheza ugenini mjini Bamako-Mali Jumapili (Februari 26) dhidi ya AS Real Bamako katika Uwanja wa Machi 26, chini ya usimamizi wa Mwamuzi kutoka nchini Botswana Joshua Bondo.

Kocha Nabi amesema amekua na zaidi ya mfumo mmoja anaoutumia dhidi ya timu pinzani katika Michezo ya Ligi Kuu na ile ya Kimataifa, hali ambayo inamuaminisha kuwa na uhakika wa kupambana popote Barani Afrika.

“Kitu bora tumetanua matumizi ya mifumo yetu na tunaweza kubadilika kulingana na mpinzani ambaye tutacheza naye kwa ubora wake, hii ni faida yetu kubwa,”

“Nimewaambia wachezaji, kuwa kitu ambacho kitatupa thamani kubwa ni kwenda kuendeleza ushindi wetu, ingawa nafahamu haitakuwa rahisi, tunapaswa kujitoa kwa kucheza kwa umakini mkubwa.” amesema Kocha Nabi

Ushindi dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo umeiweka pazuri Young Africans katika msimamo wa Kundi D, ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na alama tatu, ikitanguliwa na US Monastir ya Tunisia yenye alama nne.

TP Mazembe inashika nafasi ya nne ikiwa na alama tatu, huku AS Real Bamako ikiburuza Mkia kwa kuwa na alama moja.

Hili hapa basi jipya la Geita Golf FC
Jeshi la watu 24 kupambana Uganda