Katika hali ya kushangaza Uongozi wa Vipers SC umeanza maandalizi ya mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Simba SC, ili hali mchezo wa Mzunguuko watatu ukitarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi (Februari 25) nchini Uganda.

Miamba hiyo ya Afrika Mashariki itakutana katika mchezo wa Mzunguuko wanne mwishoni mwa juma lijalo ( Jumamosi, Machi 07), jijini Dar es salaam katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Afisa habari wa Vipers FC Kenny Muhanga, amesema pamoja na mchezo wao wa kesho kutarajiwa kuchezwa Uganda, tayari wameshaanza maandalizi ya mchezo wa wa Mzunguuko wanne, utakaopigwa jijini Dar es salaam.

Muhanga amesema wanatambua wakienda jijini Dar es salaam watapata ushirikiano kutoka kwa mashabiki wa Young Africans, kufuatia upinzani uliopo kati ya klabu hiyo na Simba SC.

Hivyo Muhanga amewaomba Mashabiki wa Young Africans kujitoa bila uwoga kuishangilai timu yao itakapocheza na Simba SC, Uwanja wa Mkapa mwishoni mwa juma lijalo Machi 07.

“Tuna uhakika tunachukua alama tatu kwa Simba SC hapa nyumbani kesho Jumamosi hatuna shaka kabisa, halafu juma lijalo tutakuwa Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa mzunguuko wanne wa Kundi C.”

“Tunaomba Sapoti kubwa kutoka kwa Mashabiki wa Young Africans, tunajuwa wao ni Wananchi na sisi pia ni timu ya Wananchi, tunajua Watatusapoti tutakapokuwa Dar es salaam.” amesema Muhanga

Vipers SC tayari imeshajikusanyia alama moja kwenye msimamo wa Kundi C, baada ya kuambulia sare ya bila kufungana na Horoya AC ya Guinea, huku Simba SC ikiambulia patupu hadi sasa ikiwa inaburuza mkia wa Kundi hilo.

Raja Casablanca ya Morocco inaongoza msimamo wa Kundi C, ikiwa na alama sita baada ya kuzifunga Vipers SC na Simba SC, huku Horoya AC ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na alama nne zilizotokana na ushindi dhidi ya Simba SC na sare dhidi ya Vipers SC.

Wanafunzi wasiofika shule kusakwa nyumba kwa nyumba
Matumizi ya mtandao wa TikTok yapigwa marufuku