Walimu nane wa shule za msingi Mkoani Mwanza wako mikononi mwa polisi wakituhumiwa kuiba zaidi ya Sh. 273 Milioni kutoka Benki ya Walimu (MCB), baada ya kuingilia (kudukua) mifumo ya benki hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa walimu hao waliiba kiasi hicho cha fedha Februari 20, 2023 kwa kujihamishia kwenye akaunti zao baada ya kudukua mifumo ya kibenki.

Kamanda Mutafungwa amesema kuwa baada ya kuwapekua watuhumiwa hao, walikutwa na fedha taslimu pamoja na mali mbalimbali zinazoaminika kuwa ni za wizi.

Aliwataja watuhumiwa hao pamoja na shule zao kwenye mabano kuwa ni Gasper Maganga (shule ya msingi Kilabela) Wilaya ya Sengerema, Marwa Mwita (shule ya msingi Nyitundu Sengerema), Masaba Mnanka (Shule ya Msingi Kilabela), Harold Madia (Bugumbikiswa), Clever Banda (Sekondari ya Nyamatongo Sengerema), Justin Ndiege (Shule ya Msingi Ishishangolo), Fredrick Ndiege (Pamba C) na Steven Sambali wa shule ya msingi Nyangongwa.

Adel Amrouche akabidhiwa mikoba Taifa Stars
Jamie Carragher amlaumu Pep Guardiola