Ukaguzi wa Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikalu – CAG, umebaini kuwa Shilingi 11.07 bilioni Serikali, hazikuwekwa katika akaunti za benki na wakusanyaji wa mapato kutoka Mamlaka 98 za Serikali za Mtaa.
Hayo yamebainishwa hii leo Machi 29, 2023 na Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali – CAG, Charles Kichere wakati wa akikabidhi ripoti ya Taasisi hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amesema Serikali za Mitaa ndiyo nguzo ya uendeshaji wa shughuli za eneo husika, lakini hata hivyo amebaini baadhi ya fedha hazikuwasilishwa benki baada yakukusanywa.
Amesema, “Mawakala wa ukusanyaji mapato katika mamlaka 10 za Serikali za Mitaa hawakuwasilisha Shilingi 4.12 bilioni kwenye benki husika,” huku akiwataka wakurugenzi nchini kuhakikisha fedha zote zinawekwa benki kama sheria inavyoelekeza.