Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema endapo kila Mtanzania angekuwa akifanya kazi na kusimamia majukumu yake ipasavyo changamoto mbalimbali ikiwemo za uwepo wa watoto wa mtaani sizingekuwepo katika kiwango kikubwa.

Kasesela ameyasema hayo nyumbani kwake mjini Iringa wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 na kuongeza kuwa usimamiaji wa majukumu na uwajibikaji wenye kujali maisha ya watu wengine husaidia kuondosha sintofafamu zilizopo kwenye jamii.

Richard Kasesela

Amesema, “ Utakuta mtu ana mtoto au wazazi wana mtoto lakini hawamtaki na ukichunguza kwa makini huwezi pata majibu yenye mashiko, mzazi anamuacha mtoto ajihangaikie hampi uelekeo wa maisha, hampi elimu hapo unatarajia nini Kama si kuzalisha watoto wa mitaani.”

Aidha, Kasesela ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), NEC amesema kila mwanajamii anatakiwa kuishi maisha ya kujitoa kwa ajili ya wengine, kusimamia kila hatua za maisha kwa watoto wao ili kusaidia ukuaji wa Taifa lenye mwelekeo sahihi wa kizazi chake na kupunguza adha zilizopo katika jamii.

Zubery Katwila atamba kuifumua Simba SC ASFC
Waarabu wanaziwinda Simba SC, Young Africans CAF