Meneja wa kikosi cha Arsenal, Mikel Arteta amesema kwa sasa anataka wachezaji wake waendelee kupambana ilikuendeleza wimbi la ushindi katika Michezo ya Ligi Kuu ya England, huku ikisalia michezo tisa kabla ya msimu kumalizika.

Arsenal, ambayo iliibanjua Leeds United kwa mabao 4-1 nyumbani, Jumamosi (April Mosi), kwa sasa inaongoza msimamo wa Ligi ya England kwakufikisha alama 72, baada ya kucheza michezo 29, ikishinda 23, Sare tatu na kufungwa tatu.

Kwenye mchezo huo, mabao mawili ya Arsenal yalifungwa na Mshambuliaji kutoak nchini Brazil Gabriel Jesus, ambaye alikuwa akirejea kutoka kwenye majeraha ya muda mrefu.

Arteta amekiri kwamba hakutegemea kuona kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake kwa sababu hawakuwa na muda mrefu tangu waliporudi kutoka kwenye timu zao za taifa na hawakupata muda mwingi wa kufanya mazoezi pamoja.

“Tunafanya kile ambacho tunakiweza, kila mchezaji alionekana akihitaji kushinda, tumeshinda mchezo kwa namna nzuri ya kucheza mpira unaovutia, jambo ambalo ni muhimu sana.”

“Jesus alikuwa akipambana sana kuhakikisha anarudi kwenye hali yake na alikuwa akifanya hivyo kwa miezi mitano iliyopita, alikuwa na haki ya kuanza kwenye mchezo na kiwango alichoonyesha pia kimedhihirisha hilo,” amesema Arteta.

Arsenal itavaa Liverpool (April 09), kabla ya kukutana na West Ham (April 16), kisha Southampton (April 21), na baada ya hapo itakuwa na kazi kubwa ya kufanya kwenye mchezo dhidi ya Manchester City na Chelsea, ambazo ikishinda zote itakuwa na uhakika wa asilimia zaidi ya 90 za kutwaa ubingwa msimu huu 2022/23.

Mzee Museveni alikataa nisiwakabili wahuni Kenya: Muhoozi
Wanahabari watanzania wanyakua tuzo za Merck Foundation