Meneja wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City Pep Guardiola amesema ushindi wa mabao 4-1, alioupata dhidi ya Liverpool unapaswa kuelekezwa kwa wachezaji wake waliopmbana kwa dakika 90 za mchezo huo.

Guardiola amesema pamoja na kikosi chake kushinda, wachezaji walionyesha viwango bora na kuufanya mchezo kuwa mzuri ambao haujawahi kutokea katika kipindi cha miaka saba akiwa kama mkuu wa Benchi la Ufundi la Manchester City.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania amesema kikosi chake kilitandaza kandanda safi huku akimsifu Jack Grealish na uwepo wa Julian Alvarez, aliyesajiliwa katika usajili unaotajwa kuwa ni wa kipekee.

Pep ambaye alianza kufanya kazi Etihad Stadium mwaka 2016, amesema ushindi mkubwa ambao amewahi kushinda mwaka ni kipindi ameiongoza timu mataji manne ya Ligi Kuu, manne ya Kombe la Ligi na Kombe la FA.

Baadhi ya ushindi huo mkubwa ni pamoja na kipigo cha mabao 6-0 dhidi ya Chelsea mwaka 2019, ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Watford mwaka huo huo na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid mwaka 2020 katika mchezo uliopigwa Bernabeu.

Mchezo mwingine ni katika ushindi wa mabao 6-0 katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Burnley.

“Liverpool huwa tishio inapofanya mabadiliko lakini timu yangu ilicheza vyema na kuidhibiti huku ikipata matokeo mazuri na kuufanya mchezo kuwa miongoni mwa mechi bora katika kipindi cha miaka saba”.

“Wachezaji walijua nini wanafanya na ndio maana hawakucheza vibaya, bao la kwanza liliwaongezea nguvu na kupata ushindi mwingine baada ya matokeo kuwa mabao 2-1,” amesema Guardiola.

Timu ya Taifa ya Riadha yaingia kambini
Majaliwa awapa neno Wakuu wa mikoa, ataka utekelezaji