Uongozi wa Klabu ya Young Africans umetoa neno la shukurani kwa Mashabiki na Wanachama waliojitokeza Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi-DR Congo, katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Barani Afrika, uliopigwa jana Jumapili (April 02).
Young Africans iliyokuwa ugenini ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji wao TP Mazembe, bao la ushindi likifungwa na Kiungo Mshambuliaji Farid Muss Malik katika kipindi cha pili.
Kupitia Kurasa za Mitandao ya Kijamii za klabu hiyo, Uongozi umewasilisha neno hilo la shukurani kwa Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo ambao wengine walilazimika kusafiri kutoka jijini Dar es salaam kwa usafiri maalum wa Basi.
“Shukrani na pongezi kwa Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Young Africans SC Congo mmekuwa watu wema na msaada mkubwa kwetu???”
“Wote waliosafiri kuja kutupa nguvu na sapoti mtaishi milele kwenye historia ya Klabu yetu na kuwa sehemu ya mafanikio yetu? pamoja na wote waliokuwa wanatuombea na kutusapoti wakiwa nyumbani??”
Hakika ???? ??????? lilihamia Congo??” imeeleza taarifa iliyochapishwa katika kurasa za mitandao ya kijamii za Young Africans
Ushindi wa 1-0 dhidi ya TP Mazembe umeifanya Young Africans kumaliza kinara wa Kundi D, ikifikisha alama 13 sawa na US Monastir iliyoifunga AS Real Bamako 2-1 jana Jumapili (April 02) nchini Tunisia.
Kwa mantiki hiyo Young Africans itakutana na moja ya timu zilizomaliza nafasi ya pili katika Kundi A, B na C Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Timu hizo ni Rivers United ya Nigeria, Pyramids ya Misri au USM Alger ya Algeria.