Baada ya kuukosa mchezo wa jana Jumapili  (April 02) dhidi ya TP Mazembe kutokana na changamoto za usafiri, imefichuka kuwa kiungo mshambuliaji kutoka Burkina Faso na Klabu ya Young Africans Stephane Aziz Ki amepewa programu maalum ya kuhakikisha anakuwa FIT kwa ajili ya mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Geita Gold.

Young Africans itaikabili Geita Gold FC katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es Salaam Jumamosi (April 08), ikiwa na malengo la kutetea ubingwa wa ASFC iliyoutwaa msimu uliopita kwa kuichapa Coastal Union mjini Arusha.

Meneja wa Young Africans Walter Harrison amesema: “Aziz Ki alikosekana kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe kwa sababu za changamoto za usafiri lakini alipewa program maalumu za mazoezi kuhakikisha anakuwa fiti kuelekea mchezo dhidi ya Geita Gold.”

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu wote tunakumbuka mchezo wa mwisho dhidi ya Geita Gold ulivyokuwa na ushindani na sasa tuna vita nyingine ya Robo Fainali nasi kama mabingwa watetezi ni lazima tuhakikishe tunashinda na kwenda hatua inayofuata.”

Binti asimulia mkasa wa kuachika, ataja siri za ushindi
Kocha Esperance de Tunis aihofia Simba SC