Kikosi cha Young Africans kimeanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam kikitokea Lubumbashi-DR Congo ambako jana Jumapili (April 02) kilicheza mchezo wa mwisho wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Young Africans inarejea Dar es salaam ikiwa na furaha ya ushindi wa 1-0, bao likifungwa na Farid Mussa Malik aliyeingia kipindi cha pili akichukuwa nafasi ya Kiungo Mudathir Yahya Abbas.

Vyanzo vya habari vya Young Africans vimethibitisha kikosi cha klabu hiyo kuanza safari kutoka mjini Lubumbashi kuelekea jijini Dar es salaam.

Baada ya mchezo huo wa CAF, Young Africans itakabiliwa na mpambano wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Geita Gold FC utakaopigwa Jumamosi (April 08), Uwanja wa Azam Complex Chamazi, kisha itaisubiri Kagera Sugar jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu na April 16 itapapatuana na Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Manchester City yamvuruga Jurgen Klopp
Akpan aahidi kurudi kwa kishindo Simba SC