Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans van Pluijm amesema malengo yao msimu huu ni kuwa mabingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’, FA bila kujali watacheza na timu gani.

Singida Big Stars juzi Jumapili (April 02) ilikuwa ya kwanza kutinga Nusu Fainali ya michuano hiyo kwa ushindi wa mabao 4-1, dhidi ya Mbeya City na sasa itakutana na mshindi wa mchezo kati ya bingwa mtetezi Young Africans dhidi ya Geita Gold FC utakaochezwa Jumamosi (April 08).

Pluijm amesema amefurahishwa na wachezaji wake ambao walicheza kwa kujituma dhidi ya Mbeya City hasa kipindi cha kwanza walichofunga mabao matatu.

“Tulikuwa bora kwenye kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili hatukucheza vizuri pengine kwa kuwa tulikuwa mbele kwa mabao hayo matatu lakini vijana wangu walicheza vizuri na kupambana sababu Mbeya City siyo timu dhaifu,” amesema Pluijm.

Amesema amekiandaa kikosi chake kupambana na timu yoyote hivyo anajua hatua inayokuja huenda akakutana na Young Africans, wapo tayari kukabiliana nao, na anaamini watapata ushindi sababu hakuna timu wanayoihofia.

Amesema anakubali kwa sasa Young Africans ni timu bora na inafanya vizuri kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ikitinga hatua ya Robo Fainali lakini haya ni mashindano mengine hivyo hawaihofii watapambana kutafuta ushindi na dakika 90 ndio zitatoa majibu.

Samsung yasogeza mazuri ya simu za Galaxy S23 Series kupitia wahamasishaji maarufu
Kocha PSG amtetea Lionel Messi