Rasmi Klabu ya Kagera Sugar imethibitisha kuvunja mkataba na Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Abdul Aziz Makame, ambaye alikua akiripotiwa kuwa katika matatizo na Uongozi wa Klabu hiyo ya mkoani Kagera.

Kagera Sugar imethibitisha kuachana na kiungo huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za Young Africans na Namungo FC zote za Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa kutoa taarifa kwa umma

Taarifa hiyo imeeleza: Klabu ya Kagera Sugar tunapenda kuujulisha umma na wanamichezo wote kwamba leo Tar 4 April 2023 tumefikia makubaliano ya Kuvunja Mkataba na aliyekuwa mchezaji wetu Abdul Aziz Makame.

Abdul Aziz Makame alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu yetu mwaka 2022 mwezi wa Saba.

Klabu inamshukuru sana MAKAME kwa huduma yake aliyoitoa kwa kipindi chote cha msimu mmoja alipokuwa akiitumikia klabu hii na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya ya soka huko aendako.

Imetolewa na.

Idara ya Habari na Mawasiliano

KAGERA SUGAR FOOTBALL CLUB

04 APRIL 2023

Kocha Simba SC ashusha Presha CAF
CPB yanunua Mazao ya Bilioni 9.6, yazalisha tani 1000