Bunge limewachagua wenyeviti watatu ambao watasaidia kuongoza vikao vya bunge kwa maelekezo ya Spika wa Bunge au Naibu Spika kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Bunge.

Akizungumza bungeni, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Akcson amesema utaratibu wa kuwapata wenyeviti wa bunge umewekwa katika Kanuni ya 13 ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Aidha amesema kuwa katika chaguzi zinazofanyika bungeni iwapo idadi ya wagombea inalingana na nafasi zilizopo na vigezo vinavyohitajika vimetimizwa basi wagombea hao wanapita bila kupigwa.

Waliothibitishwa kuwa wenyeviti ni pamoja na Najma Murtaza Giga ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum na Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Daniel Baran Sillo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

Mwingine aliyechaguliwa ni David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Jimbo la Mufundi Kusini na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo

Jean Baleke: Tuna kazi kubwa mbele yetu
UN walaani ukiukwaji wa haki za binadamu Sudan Kusini