Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Augustine Okrah amesema yupo tayari kuikabili Young Africans April 16, baada ya kurejea mazoezini kwa mara ya kwanza jana Jumanne (April 04).

Okrah amerejea katika mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake wa Simba SC baada ya kuwa nje ya uwanja kwa majuma manne akiiguza kidole, ambacho alivunjika kwenye mchezo wao wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Al Hilal Omdurman.

Kiungo huyo amesema yupo FIT na ameshaanza mazoezi ya kuelekea mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Ihefu FC utakaopigwa keshokutwa Ijumaa (April 07), Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

“Namshukuru Mungu naendelea poa sasa baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda, nimesharuhusiwa kuanza mazoezi na nimeungana na timu baada ya timu kurejea kutoka mapumziko,”

“Natamani kupata nafasi ya kucheza michezo ya ligi zilizobaki ili kujiweka katika mazingira mazuri kutokana na kukosekana na muda mrefu na kuhusiana na ratiba iliyopo kuna mchezo dhidi ya Young Africans Aprili 16 naitamani sana ukweli, naomba kocha anipe jezi kwenye mchezo huo,” amesema Okrah

Okrah amesema alipokuwa nje ya uwanja muda mwingi alikuwa anautumia kufanya mazoezi na kuangalia michezo ya timu yake na wapinzani kila anapopata nafasi, hivyo anatambua ubora wa Young Africans na mapungufu yao.

Kiungo huyo mshambuliaji alijiunga na Simba SC dirisha kubwa la usajili amesema amerudi wakati sahihi ambao timu bado imebakiza michezo sita ya ligi ambayo amekiri kutamani kupata nafasi ya kucheza ili iweze kumrudisha kwenye ushindani.

Maagizo sita ya Waziri Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI
TARI – Dakawa yapatiwa Milioni 30 kusafisha Mbegu za asili za Mpunga