Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Shilingi 8.64 Trilioni zimetolewa na Serikali kwa ajili ya kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo itakayoimarisha uchumi wa nchi na maendeleo ya watu hadi kufikia Januari, 2023 ambayo ni Reli, Barabara, Viwanja vya Ndege, Huduma za Jamii na Nishati.

Majaliwa ameyasema hayo leo hii leo Aprili 5, 2023 wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024 bungeni jijini Dodoma.

Amesema, Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 762.99 kutekeleza mradi wa ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR) ambapo kipande cha Dar es Salaam – Morogoro chenye urefu wa kilomita 300 utekelezaji umefikia asilimia 97.91.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Majaliwa ameongeza kuwa, kipande cha Morogoro – Makutupora (km 422) kimefikia asilimia 92.23, kipande cha Mwanza – Isaka (km 341), asilimia 25.75, kipande cha Makutupora – Tabora (km 371) asilimia 4.59 na kuanza kwa ujenzi wa kipande cha Tabora – Isaka (km 165) na Tabora – Kigoma (Km 506).

Kuhusu mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (MW 2,115) Waziri Mkuu amesema Serikali imetoa takribani shilingi bilioni 869.93 kwa ajili utekelezaji wa mradi huo ambao umefikia asilimia 83.

Aidha, amesema zoezi la ujazaji maji katika bwawa hilo lilizinduliwa rasmi na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 22 Desemba 2022, ambapo hadi kufikia Februari, 2023 kiwango cha maji kimefikia mita 134.39 kutoka usawa wa Bahari ikilinganishwa na kiwango cha mita 163 kinachohitajika ili kuanza uzalishaji.

Fiston Mayele aitamani Simba SC April 16
Watu 805 wapewa elimu ugonjwa wa Marburg Magereza