Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa amesema uboreshaji wa Shirika la Ndege Tanzania uligharimu Shilingi 20.52 Bilioni ambapo shughuli zilizofanyika katika utekelezaji wa mradi huo ni pamoja na kulipa sehemu ya gharama za ununuzi wa ndege tano.

Majaliwa ameyasema hayo hii leo Aprili 5, 2023 wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024 Bungeni jijini Dodoma.

Amesema, kati ya hizo, ndege moja ni aina ya Boeing 767-300F ya mizigo, ndege mbili aina ya Boeing 737-9, ndege moja aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na ndege moja aina ya De Havilland Dash 8-Q400. Ndege nne kati ya hizo zinatarajiwa kuwasili nchini kabla ya Novemba, 2023.

“Ndege moja ya mizigo inatazamiwa kuwasili nchini hivi karibuni. Kuwasili kwa ndege hizo kutasaidia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutanua mtandao wa safari za ndani na nje ya nchi na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za uchumi kama utalii, biashara na kilimo,” amesema Waziri Mkuu.

Aidha, ameongeza kuwa shilingi 30.39 Bilioni zimetolewa na Serikali, ili kulipa fidia wananchi 7,486 kati ya 9,122 wanaopisha eneo la mkuza wa mradi wa ujenzi wa bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda), hadi Tanga (Tanzania), lenye urefu wa km 1,443

Serikali yasaini huduma za Binadamu, operesheni za dharura SADC
Uaminifu sekta ya Madini utakuza uchumi wa Taifa: Waziri Biteko