Serikali imeunda Madawati 1,393 ya ulinzi na usalama wa mtoto katika shule za msingi na sekondari ili kupinga ukatili dhidi ya watoto shuleni na nje ya shule, katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwenye mikoa ya Rukwa, Arusha, Tanga, Dar es Saalam, Pwani, Shinyanga, Dodoma na Geita.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa hii leo Aprili 5, 2023, wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024 bungeni jijini Dodoma.

Amesema, mabaraza 560 ya watoto yameundwa ili kutoa fursa kwa watoto kutoa maoni yao kwa uhuru na kuwajengea uwezo wa kujiamini, kujieleza na kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wao na kuwasisitiza viongozi wa Serikali, dini, kimila na vyama vya siasa kukemea ushiriki wa jamii katika matendo yasioendana na mila, tamaduni na desturi za Watanzania.

Amesema, “hii ni pamoja na wazazi na walezi wote kushirikiana na Serikali katika makuzi na malezi bora ya watoto yatakayowaepusha na vitendo viovu. Serikali imeendelea kuhamasisha jamii kushiriki katika ulinzi na usalama wa mtoto ili kutokomeza ukatili dhidi yao.”

Serikali yaendelea kulipa hisa umiliki Bomba la Mafuta EA
Serikali yasaini huduma za Binadamu, operesheni za dharura SADC