Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema wajumbe 555 wa Kamati za Usimamizi wa Maafa na Waratibu wa Maafa walipatiwa mafunzo ya kuimarisha uwezo wa utendaji kazi katika mikoa ya Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara na Singida.

Majaliwa ameyasema hayo leo hii leo Aprili 5, 2023 wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024 bungeni jijini Dodoma.

Mafunzo ya uokoaji wakati wa ajali za Majini.

Amesema, “pia wavuvi 344 katika mwambao wa Ziwa Victoria na vijana 40 wa kujitolea katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Songwe na Tabora walipata mafunzo ya uokoaji, yaliyowaongezea uwezo wa kukabiliana na maafa kwa wakati,” amesema.

Majaliwa ameongeza kuwa, katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaendelea na ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Usimamizi wa Maafa jijini Dodoma na kuimarisha maghala ya vifaa vya misaada ya kibinadamu kwa kuongeza vifaa na kuendelea kutoa misaada kwa waathirika wa maafa.

Mikataba ya Bilioni 284.14 yasainiwa ujenzi Skimu za umwagiliaji
Rais UEFA azugumzia kashfa ya Waamuzi, Barca