Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameliomba Bunge liidhinishe shilingi 173,733,110,000 ambapo kati ya fedha hizo, sh. 121,364,753,320/- ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 52,368,356,680 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo kwa Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake.
Majaliwa ametoa ombi hilo hii leo Aprili 5, 2023 wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024 bungeni jijini Dodoma.
Aidha, Majaliwa pia ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya shilingi. 165,627,897,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo sh. 160,458,877,000/- ni za matumizi ya kawaida na sh. 5,169,020,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.