Rais wa Heshima na Mwekezaji Mwenza wa Simba SC Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema anaamini hakuna njia ya mkato kwa klabu hiyo kufikia malengo ya kutwaa ubingwa Barani Afrika, zaidi ya kukutana na Vigogo vya soka Barani humo.

Mo Dewji amejinasibisha hivyo baada ya Simba SC kuangukia mikononi mwa Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika Wydad Casablanca katika mchezo wa Robo Fainali ya michuano hiyo.

Simba SC ilimfahamu mpinzani huo baada ya kupangwa kwa Droo ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika usiku wa jana Jumatano (April 05) mjini Cairo nchini Misri.

Kutokana na hali hiyo Mo Dewji ameandika ujumbe katika kurasa zake zote za mitandao ya kijamii akionesha Simba SC inapaswa kukutana na vigogo vya soka Afrika ili kufikia malengo yake ya kuwa Bingwa wa bara hilo.

Mo Dewji ameandika: Njia pekee ya kusonga mbele ni kuwashinda mabingwa! Tunakuja Simba!

Simba SC ilitinga Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ikifikisha alama 09 nyuma ya Raja Casablanca ya Morocco iliyomaliza michezo ya Kundi C ikiwa na alama 16, huku Horoya AC ya Guinea ikimaliza na alama 07 na Vipers SC ya Uganda inaburuza mkia wa Kundi hilo kwa kuwa na alama 02.

Young Africans: Tutalipa kisasi kwa River United
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo April 6, 2023