Kampuni ya Roc Nationa inayomsimamia Romelu Lukaku imekuja juu baada ya Mshambuliaji huyo kutoka Ubelgiji anayekipiga Inter Milan kufanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki wa Juventus.
Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa Kombe la Italia, Inter Milan ilipocheza dhidi ya Juventus juzi Jumanne (April 04) mchezo huu ukimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mbali na kubaguliwa Lukaku alilimwa kadi nyekundu kutokana na staili yake ya ushingiliaji baada ya kusawazishia bao kwa mkwaju wa Penati dakika ya 95 ya mtanange huo.
Bao la Juventus liliwekwa kimiani na Juan Cuadrado ambaye alipewa kadi nyekundu baadae kabla ya kipa wa Inter, Samir Handanovic naye alilimwa kadi nyekundu.
Lakini kwa upande wa Lukaku alilimwa kadi mbili za njano baada ya kushangilia kwa staili ya kuwanyamazisha mashabiki baada ya kumwimbia wimbo wa kibaguzi wakimwita ‘nyani”
Sasa vitendo hivyo vya kibaguzi vimewaudhi wawikilishi wake wanaomiliki Kampuni ya ‘Roc Nation’ kutoka Marekani ambayo inayosimamia masuala ya michezo, kampuni hiyo imeomba mamlaka kutoka Italia ichukue hatua dhidi ya Juventus.
Roc Nation iliandika barua yenye ujumbe mzito kutokana na tukio hilo lililotokea kwenye mchezo huo wa Kombe la Italia wakilaani vitendo kubaguzi. Ujumbe huo vya ulisomeka hivi;
“Matamshi ya kibaguzi usiku dhidi ya Romelu Lukaku kutoka kwa mashabiki wa Juventus, yalikuwa ya kuchukiza na hayawezi kukubalika, Lukaku alifunga bao kwa mkwaju wa penalti, kabla na baada akatendewa vitendo vya kibaguzi, Lukaku siku zote anashangilia hivyo, Mwamuzi anampa kadi nyekundu, Lukaku anastahili kuombwa radhi, ligi inatakiwa kulaani vitendo vya kibaguzi kama hivyo hususan kwa mashabiki kwa Juventus.”