Beki wa Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich Benjamin Pavard, hajui kuhusu hatma yake ndani ya kikosi cha mabingw ahao ingawa imeelezwa kuwa Meneja mpya Thomas Tuchel ana mpango naye.

Mkataba wa Pavard na FC Bayern Munich unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na bado hajafanya mazungumzo na Uongozi wa klabu hiyo ambayo ilirejea kileleni mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuiadhibu Borussia Dortmund kwa 4-2.

Beki huyo kutoka nchini Ufaransa ameanza kutajwa na klabu tofauti za Ulaya kama FC Barcelona ya Hispania na Manchester United ya England.

Inaelezwa kuwa, Pavard amesema hajui hatma yake kikosini hapo kwani mazungumzo yalianza katia yake na Uongozi wa juu, lakini yakasimama na huenda yakaanza tena.

Meneja mpya wa FC Bayern Munich Tuchel amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Ujerumani akisema: “Pavard ni mchezaji ambaye amekuwa hapewi nafasi, najua ni mchezaji mkubwa tena mwenye kiwango cha juu, ana nidhamu na ni mchezaji wa daraja la juu.”

“Ninaamini ni suala la muda tu yeye kujiamini, ninaamini tutafanya kitu kizuri.”

Ansu Fati hatarini kuondoka FC Barcelona
Senzo: Ninaiona Young Africans Nusu Fainali