Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameungana na viongozi na wananchi mbalimbali katika kumbukizi ya Miaka 51 ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Ibada na kumbukizi ya miaka hiyo 51 ya kifo cha Abeid Amani Karume imefanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, CCM – Kisiwandui Zanzibar, hii leo leo Aprili 7, 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar Zanzibar hii leo Aprili 7, 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwasili Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – Kisiwandui Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini na Chama katika dua ya pamoja ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume katika kumbukizi ya miaka 51 ya kifo chake.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Wawili wanaswa na vipande 45 vya meno ya Tembo
Saba washikiliwa na Polisi kwa mauaji, ufukuaji makaburi